Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO latoa wito kwa Libya na NATO kuyalinda maeneo ya kale

UNESCO latoa wito kwa Libya na NATO kuyalinda maeneo ya kale

Shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limetoa wito kwa pande zinazopigana nchini Libya kuyalinda maeneo mawili ya kitamaduni baada ya moja kati yao kushambuliwa huku lingine likisemekana kulengwa na mashambulizi ya jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa mji wa kale wa Ghadamès unaripotiwa kushambuliwa kwa mabomu na wanjeshi wa serikali mwishoni mwa juma huku NATO ikikataa kukana madai kuwa ina nia ya kuushambilia mji wa Kirumi wa Leptis Magna ulio mashariki mwa Tripoli ulio na maghala ya silaha za serikali.

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova hii leo ametoa wito kwa pande zinazopigana nchini Libya kuhakikisha kuwa mji wa kale wa Ghadamès umepewa usalama.