Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiongozi wa zamani wa Intarahamwe afikishwa mahakama ya ICTR

Kiongozi wa zamani wa Intarahamwe afikishwa mahakama ya ICTR

Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Rwanda wanaojulikana kama Interahamwe waliotekeleza mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 amehamishiwa kwenye mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa iliyoko Arusha Tanzania.

Bernard Munyagishari Rais wa zamani wa Intarahamwe eneo la Gisenyi Rwanda alikamatwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi uliopita.

Munyagishari anadaiwa kuwakusanya, kuwapa mafuunzo na kuwaongoza waasi wa Intarahamwe katika mauaji ya kimbari na kuwabaka wanawake wa Kitutsi na wengineo kati ya Aprili na Julai mwaka 1994.

Mtuhumiwa huyo alihamishiwa kwenye mahakama ya ICTR juni 14 mwaka huu na anatarajiwa kupanda kizimbani kukabiliwa na makosa ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwemo ubakaji.

Alikamatwa Mai 25 katika operesheni maalumu iliyoendeshwa na majeshi ya serikali ya Congo kwa ushirikiano na ofisi ya mwendesha mashitaka na upelelezi ya Congo iliyoko Kachanga Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa Congo.