Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO ina mchango mkubwa katika kuwalinda wanawake na watoto:Kikwete

ILO ina mchango mkubwa katika kuwalinda wanawake na watoto:Kikwete

Kikao cha 100 cha shirika la kazi duniani ILO kinaendelea mjini Geneva kikijadili mada mbalimbali za kuhakikisha huduma muhimu kwa jamii zinapatikana.

Mada kuu kabisa ni kuwalinda makundi yasiyojiweza hususani wanawake na watoto ili waweza kupata huduma muhimu, kutobaguliwa, kutengwa na kutosalia masikini.

Mkutano huo uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali unasisitiza umuhimu wa kutoa fursa hasa za ajira bora kwa wote, kuheshimu haki za kazi, kutoa ulinzi unaohitajika kwa jamii na kuruhusu mijada kwa jamii ambayo itakuwa na manufaa. Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya muuungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anasema ILO inajukumu muhimu sana duniani.

(SAUTI YA JAKAYA KIKWETE)