Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo ya kiangazi ya Gaza imeanza rasmi leo:UNRWA

Michezo ya kiangazi ya Gaza imeanza rasmi leo:UNRWA

Watoto 250,000 wa Kipalestina wanashiriki katika mashindano ya tano ya kiangazi yanayofanyika kila mwaka , yajuliknayo kama michezo ya kiangazi ya Gaza, ambayo imeaanza rasmi hii leo , kwa mfumo wa olympiki wa mbio za kupokezana vijiti kwenye Ukanda wa Gaza.

Huu ni mwaka wa tano ambapo shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA linaandaa michezo hiyo ambayo inajumuisha michezo mbalimbali , sanaa, utamaduni na shughuli za kielimu.

UNRWA inasema michezo hiyo inasaidia kuendeleza vipaji vya watoto, kuwapa nafasi ya kujieleza na kuwafunza kuheshimiana. Filippo Grandi ni kamishina mkuu wa UNRWA.

(SAUTI YA FILLIPO GRANDI)