Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waipongeza mipango ya Chad ya kutaka kumaliza matumizi ya watoto jeshini

UM waipongeza mipango ya Chad ya kutaka kumaliza matumizi ya watoto jeshini

Afisa wa Umoja wa Mataifa ameipongeza mipango iliyotiwa saini na serikali ya Chad ili kumaliza matumizi ya watoto kwenye majeshi yake ya ulinzi na usalama, huku ikiainisha hatua za baadaye za kuhakikisha tatizo la askari watoto linamalizika kabisa.

Bi Radhika Coomaraswamy ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa kwa ajili ya watoto kwenye maeneo ya vita amesema kutiwa saini kwa mipango hiyo kunaashiria ari ya kisiasa na wajibikaji wa serikali ya Chad kusonga mbele kwa kutokomeza ukiukwaji huo mkubwa wa haki za watoto. Amesema hiyo ni hatua kubwa lakini bado kuna changamoto mbele . Coomaraswamy ameyasema hayo kwenye hafla maalumu ya kutia saini mipango hiyo kwenye mji mkuu wa Chad N’djamena. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)