Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika vita vya ukimwi Tanzania kuongeza elimu, madawa na utafiti:Dr Bilal

Katika vita vya ukimwi Tanzania kuongeza elimu, madawa na utafiti:Dr Bilal

Serikali ya Tanzania inasema pamoja na kupiga hatua katika vita dhidi ya ukiwmi bado ina safari ndefu ingawa zaidi ya asilimia 50 ya waathirika wanapata dawa za kurefusha maisha.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Dr Mohammed Gharib Bilal aliyezungumza kwa kina na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa Flora Nducha nia yao ni kufikia maambukizi sufuri, vifo sufuri na unyanyapaa sufuri dhidi ya ukimwi.

Msisitizo pia inaweka kwa kina mama ambao inaonekana hawana maamuzi makubwa ikilinganishwa na wanaume katika gonjwa hilo hatari. Dr Bilal anaanza kwa kufafanua hatua zilizopigwa na taifa hilo la Afrika ya Mashariki katika mapambano ya ukimwi.

(MAHOJIANO NA DR BILAL)