Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM na hali kwenye jimbo la Kordofan Kusini

Mashirika ya UM na hali kwenye jimbo la Kordofan Kusini

Zaidi ya watu 53,000 wamekimbia makwao katika jimbo la Kordofan kusini nchini Sudan kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya wanajeshi kutoka kaskazini na wale kutoka kusini. Mashirika ya kutoa misaada ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa yameshindwa kuyafikia maghala yao kutokana na kuwepo ukosefu wa usalama.

Nalo shirika la WHO linasema kuwa ghala lake na ofisi zimevunjwa na madawa yenye thamani ya dola 180, 000 kuporwa . Sasa mashirika hayo yanatoa wito kwa utawala katika eneo hilo kuruhusu usafiri wa barabara na anga ili waliokimbia makwao waweze kupelekewa misaada. Melissa Fleming ni kutoka shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR:

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)