Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame kwenye upemba wa Afrika wayaweka hatarini maisha ya wengi:FAO

Ukame kwenye upemba wa Afrika wayaweka hatarini maisha ya wengi:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linaonya kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kwenye upembe wa Afrika inatarajiwa kuongezeka wakati athari za ukame zikiendelea kushuhudiwa likiwemo pia suala la kupanda kwa bei ya mafuta na chakula . FAO inasema kuwa kwa sasa idadi kubwa ya watu inakabiliwa na utapiamlo nchini Djibouti, Ethiopia, Kenya na Somalia na ambao kwa sasa wanahitaji usaidizi wa dharura. George Njogopa anaripoti:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)