Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzuia uchafuzi wa hewa kunaweza kupunguza kuongezeka kwa joto duniani

Kuzuia uchafuzi wa hewa kunaweza kupunguza kuongezeka kwa joto duniani

Ikiwa hatua za haraka zitachukuliwa katika kupunguza gesi chafu zikiwemo za Carbon na Methane inaweza kusaidia kupunguza kupannda kwa viwango vya joto na pia kudumisha kupanda kwa joto kwa chini ya nyusi mbili na hata nyusi 1.5.

Kulingana na maelezo mapya hali hiyo itachangia na kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa na kuyeyuka kwa barafu iliyo ardhini na pia baharini. Hatua za haraka pia zinaweza kuchangia katika kuzuia kuyeyuka kwa barafu kwenye milima na pia kupunguza kuongezeka kwa joto ambako kumetabiriwa katika eneo la Arctic miaka kadha inayokuja.

Utafiti huo umeendeshwa kwa ushirikiano kati ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na lile na utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.