Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA haitopunguza miradi yake kwa wakimbizi Palestina

UNRWA haitopunguza miradi yake kwa wakimbizi Palestina

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA Filippo Grand amekanusha madai kwamba shirika hilo litapnguza programu zake kwa Wapalestina kama ilivyoripotiwa.

Mkuu wa UNRWA ameyasema hayo wakati Rais wa bunge la Ulaya Jerzy Buzek akiwa katika ziara ya kwanza kabisa kwenye Ukanda wa Gaza.

Bwana Grandi amesema kuwa wakati huu UNRWA ipo katika hofu kwa kuwa inapungukiwa fedha kwa ajili ya mipango yake lakini inazungumza na wahisani kujaribu kutatua tatizo hilo la fedha.

(SAUTI YA GRANDI)

Hatutokata mipango yetu. Hakuna suluhisho la suala la wakimbizi, tutakataje programu zetu? Bila shaka mipango yetu inategemea ufadhili na fedha hivyo wakati mwingine inabidi tujipange kutokana na fedha tulizonazo.