Mkutano wenye sura ya Umoja wa Mataifa unatazamiwa kutoa mchango mkubwa kwa dunia

13 Juni 2011

Kongamano ambalo linachukua kivuli cha Umoja wa Mataifa lililopangwa kufanyika huko Incheon, Korea lina nafasi kubwa ya kutoa mchango utaoleta ufumbuzi kwa baadhi ya mambo yanayoikabili dunia. 

Hayo ni kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa wanafunzi kwenye mkutano huo ambaye ameongeza kusema kuwa kongamano hilo linatoa fursa ya kuwepo kwa mijadala yenye tija katika jumuiya ya kimataifa.

Oliver Pase kutoka Australia ambaye anatazamiwa kuwa kama Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya habari na mawasiliano ya umma ameeleza kuwa kongamano hilo linalotazamiwa kufanyika Augsut 10 hadi 14 litawaleta pamoja kiasi cha wanafunzi 600 kutoka duniani kote.

Mkutano wa safari hii ambao ule uliopita ulifanyika huko Kuala Lumpur, unatazamiwa kuwa na zingatio lisemalo maendeleo endelevu kwa shabaya ya kusuma mbele ustawi wa binadamu katika maelewano zaidi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter