Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa UM wa mboga na matunda nchini DRC wapata manufaa makubwa

Mradi wa UM wa mboga na matunda nchini DRC wapata manufaa makubwa

 

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa mradi wa miaka mitano wa kilimo cha mboga na matunda ulioanzishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo umekuwa wa manufaa makubwa kwa kuleta faida, kuwahakikishia lishe watu na ajira kwa maelfu ya watu, wengi wakipata mara nne au tano zaidi ya pato walilokuwa wakipata awali.

Mradi huo wenye gharama ya dola milioni 10.4 uliofadhiliwa na Ubelgiji na kutekelezwa na wizara ya maendeleo ya vijijini tangu mwaka 2000 umewasidia wakulima kwenye miji ya Kinshasa, Lubumbashi , Mbaza-Ngungu, Kisangani na Likasi kuzalisha tani 330,000 za mboga kila mwaka. FAO inasema kuwa mradi huo umewasaidia watu 16,000 kupata ajira kama wakulima wadogo na wengine 60,000 katika ajira zinazohusiana na biashara ya mboga na matunda.