Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka raia kupewa usalama zaidi nchini Afghanistan

UM wataka raia kupewa usalama zaidi nchini Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umeutaja mwezi uliopita wa Mei kama uliokumbwa na mashambulizi mengi zaidi nchini humo kwa miaka ya hivi majuzi ambapo umetaka raia kupewa usalama zaidi.

Mkurugenzi wa haki za binadamu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afganistan UNAMA Georgette Gagnon amesema kuwa pande husika ni lazima ziweke juhudi katika kuwalinda raia. Taarifa zinasema kuwa raia wengi zaidi waliuawa mwezi wa Mei kuliko mwezi wowote ule tangu mwaka 2007.

Takriban raia 368 waliuawa kwenye mizozo mwezi Mei huku makundi yanayoipinga serikali yakihusika kwa asilimia kubwa ya vifo hivyo ambapo pia karibu watu 600 walijeruhiwa.