Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atembelea eneo lililokumbwa na mafuriko Colombia na kuahidi kupiga jeki

Ban atembelea eneo lililokumbwa na mafuriko Colombia na kuahidi kupiga jeki

Akitembelea eneo lililoadhiriwa vibaya na mafuriko nchini Colombia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema umoja huo uko tayari kuunga mkono juhudi za serikali kuwasaidia zaidi ya watu milioni tatu ambao wameathiriwa  hali hiyo.

 Ban amesema ameguswa mno hasa anapoona mamia ya watu wakihangaika kutokana na mafuruko hayo hivyo lazima kuonyesha moyo wa huruma na upendo kwa wananchi hao.

Katibu Mkuu huyo aliyetembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki na kukutana na rais Juan Manuel Santos Calderón ambao baadaye walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Amehaidi kuwa nyuma ya wananchi wa Colombia hasa katika kipindi hiki kigumu na

amepongeza hatua zilizoanza kuchukuliwa na serikali juu ya janga hilo