Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahofia kuendelea kwa machafuko Kordofan

Ban ahofia kuendelea kwa machafuko Kordofan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia hofu yake kuhusu kuendelea kwa machafuko kwenye jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan ambako maelfu ya watu wamelazimika kukimbia na wengine wameuawa.

Ban amezitaka pande zote husika kwenye mapigano kusitisha vita na kushirikiana na Umoja wa Mataifa na mashirikia ya kimataifa ya msaada wa kibinadamu ili kunusurua maisha ya watu na kuwasaidia walioathirika na mapigano. Pia Ban amesema bado anatiwa hofu na hali ya jimbo lingine la Sudan la Abyei. George Nogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)