Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imepiga hatua katika vita dhidi ya Ukimwi

Kenya imepiga hatua katika vita dhidi ya Ukimwi

Serikali ya Kenya imesema pamoja na kwamba bado inakabiliwa na changamoto katika vita dhidi ya Ukimwi lakini imepiga hatua kubwa.

Akizungumza na idhaa hii mkuu wa tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi nchini Kenya Profesa Alloys Orago amesema mbali na kugawa dawa za kurefusha maisha ambazo sasa zinawafikia watu wengi serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha wanafikia lengo la maendeleo la milenia linalohusu maradhi ikiwa ni pamoja na Ukimwi.

(SAUTI YA PROFESA ALLOYS ORAGO)

Katika mkutano uliomalizika siku ya Ijumaa viongozi na wawakilishi wa dunia takribani 3000 waliafikiana kupunguza maambukizi mapya ya ukimwina kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa asilimia 50 ifikapo 2015. Na wameahidi kuwa madawa ya kurefusha maisha yaani ARV’s yatafikia watu bilioni 15 mwaka 2015.