Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha hatua za kupambana na Ukimwi zilizopitishwa na viongozi wa dunia

Ban akaribisha hatua za kupambana na Ukimwi zilizopitishwa na viongozi wa dunia

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha azimio lililopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa la mipango mipya ya kukabiliana na virusi vya HIV na ukimwi.

Amesema azimio hilo lina lengio la kutokomeza ugonjwa huo ambao tayari umeshakatili maisha ya watu zaidi ya milioni 30 tangu ulipozuka miongo mitatu iliyopita. Ban amesema ametiwa moyo na nchi wanachama kwa kuafikiana na kujiwekea malengo maalumu ya kuzuia, kutibu, kuhudumia na kusaidia ifikapo 2015. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)