Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya waziri wa mambo ya ndani

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya waziri wa mambo ya ndani

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia mwishoni mwa wiki ameelezea kushtushwa kwake kufuatia mauaji ya waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo na kulaani vikali mauaji hayo akisema watu wachache wasiruhusiwe kutoa dosari mchakato wa amani.

Waziri Abdishakur Sheikh Hassan Farah ambaye pia alikuwa na jukumu la kuangalia usalama wa taifa aliuawa katika shambulio la kujitoa muhanga nyumbani kwake mjini Moghadishu siku ya ijumaa. Mwakilishi huyo balozi Augustine Mahiga amesema shambulio hilo lazima zilaaniwe kwa kila hali na wote wanaotaka kuona amani inarejea Somalia . Balozi Mahiga ametuma salama za rambirambi kwa familia ya marehemu na serikali ya mpito ya Somalia na kuwatakia nafuu ya hara majeruhi wote katika tukio hilo.

Umoja wa Mataifa unaisaidia Somalia kurejesha amani na utulivu baada ya zaidi ya miongo miwili bila serikali kufuatia kupinduliwa kwa serikali ya Mohammed Siad Barre mwaka 1991.