Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka mmoja wa machafuko Kyrgystan bado kuna idadi kubwa ya wakimbizi-UNHCR

Mwaka mmoja wa machafuko Kyrgystan bado kuna idadi kubwa ya wakimbizi-UNHCR

Ikiwa imepita mwaka mmoja tangu kutokea kwa machafuko makubwa ya kikabili nchini Krygystan ambayo yaligharimu maisha ya mamia ya watu, bado kuna kundi kubwa la  watu walisalia mtawanyikoni kutokana na kukosa makazi.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mamia kwa maelfu bado wanakabiliwa na changamoto ya kuwa wakimbizi wa ndani ambao zaidi wanakutikana katika eneo la kusin mwa nchi hiyo.

UNHCR inaweka msisitiza wa kuimarishwa kwa mifumo ya maridhiano ili kundi kubwa hilo la watu lirejea kwenye maeneo yao ya awali. Wakati wa machafuko hayo, zaidi ya watu 400 waliuwawa na wengine zaidi ya 375,000 walilazimika kukimbia makazi yao na kwenda kuwa wakimbizi.

Wakati huo huo ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imesema kuwa mamlaka za kiutawala nchini humo bado hazijishughulisha vyakutosha kuwatendea

haki waathirika wa machafuko hayo.