Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya uchunguzi nchini Ivory Coast yachapisha ripoti yake.

Tume ya uchunguzi nchini Ivory Coast yachapisha ripoti yake.

Tume ya kimataifa inayochunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast kufuatia uchaguzi wa urais uliondaliwa Novemba 28 mwaka uliopita imewasilisha ripoti yake kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Kulingana na uchunguzi wa tume hiyo ni kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za haki za bindamu vilitekelezwa nchini Ivory Coast. Inasema kuwa kati ya uovu uliotendwa unaweza kuwa uhalifu wa kivita na pia uhalifu dhidi ya ubinadamu. Ukiukaji huo wa haki za binadamu ulitekelezwa na vikosi vya usalama pamoja na washirika wao wakiwemo wanamgambo. Pia ripoti hiyo inasema kuwa watu katika maeneo ya magharibi , kusini magharibi na mjini Abidjan ndio waliathirika.