Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi kutoka ofisi ya haki za binadamu latoa ripoti kuhusu haki za binadmu nchini Misri

Kundi kutoka ofisi ya haki za binadamu latoa ripoti kuhusu haki za binadmu nchini Misri

Ujumbe kutoka afisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa uliotumwa nchini Misri kati ya tarehe 27 machi na tarehe 7 mwezi Aprili mwaka huu umetoa ripoti yake ukiguzia changamoto za haki za binadamu zinazohitaji kushughulikiwa nchini Misri.

Ripoti hiyo inasema kuwa kuna wasi wasi mkubwa hasa wakati kutakapoandaliwa uchaguzi. Pia maafisa kutoka wizara ya mambo ya kigeni nchini Misri wameelezea moyo wa serikali wa kuwa mwenyeji wa afisi ya tume ya haki za binadamu kanda ya kaskazini mwa Afrika mjini Cairo. Pia ripoti hiyo inasema kuwa kuna maandalizi kwa miradi kadha ikiwemo kufanyia mabadiliko sekta ya ulinzi na kuwapa mafunzo polisi kuhusu haki za binadamu.