Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kutathimini masuala ya ukimwi wakunja jamvi New York

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kutathimini masuala ya ukimwi wakunja jamvi New York

 

Tangu Juni 8 hadi 10 viongozi wa dunia na wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 30 walikusanyika hapa New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mkutano wa siku tatu kutathimini hatua zilizopigwa katika vita dhidi ya ukimwi, miakkati iliyopo na kasha kutoka na azimio jipya la vipi vita hivi vitaendelea.

Lengo la Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha dunia inapunguza maradhi hayo kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015 muda uliowekwa kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.

Nchi nyingi zimepiga hatua ikiwemo Tanzania lakini bado zinakabiliwa na cngamoto.

Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal na waziri wa afya wa Zanzibar Juma Duni Haji ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huu, nimeketi nao na kujadili hatua zilizopigwa, changamoto na mikakati ya Tanzania kwa ujumla kufaulu vita hivi. Kwanza Dr Bilal anaeleza hatua zilizopigwa na Tanzania.

(MAHOJIANO NA DR BILAL NA JUMA DUNI HAJI)