UM wajitolea kuisaidia Myanmar:BAN

9 Juni 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa umesimama imara na taifa la Myanmar kufuatia changamoto zinazoikumba serikali mpya.

Kupitia kwa msemaji wake Ban amesema kuwa ni bayana kuwa taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia linaendelea kukabiliwa na changamoto za muda mrefu zikiwemo za haki za binadamu, kisiasa , kijamii na kiuchumi . Kwenya taarifa yake kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mshauri wa Ban Vijay Nambiar amesema kuwa nchi hiyo imepiga hatua kidogo hasa kwa kuwaachilia wafungwa wa kisiasa na kupunguza vifungo vya wengine. Hata hivyo Ban amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kuona taifa la Myanmar likifanikiwa katika kutatua changamoto zinazolikumba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter