Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji wanaokabiliwa na kiangazi nchini Kenya waomba usaidizi

Wafugaji wanaokabiliwa na kiangazi nchini Kenya waomba usaidizi

Wafugaji katika maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Kenya wanaomba usaidizi ili kuokoa mifugo wao waliosalia na ambao kwa sasa hawatapata soko baada ya maeneo hayo kukumbwa na hali mbaya ya ukama hali iliyosababisha kuwepo ukosefu wa malisho . Serikali ya Kenya mara nyingi hununua mifugo kutoka kwa wafugaji wakati wa kiangazi ili kuhakikisha kuwa wamepata pesa za kuwakimi kabla mifugo hao hawajafariki.

Kwa sasa mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo shirika la kuratibu masuala ya kibindamu OCHA , shirika la kilimo na mazao FAO na pia la kimataifa la uhamiaji IOM yako kwenye wilaya ya Moyale iliyo kaskazini mwa Kenya kukadiria athari zilizosababishwa na kiangazi hicho.