Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lajadili ukiukaji wa haki Libya

Baraza la haki za binadamu lajadili ukiukaji wa haki Libya

Serikali ya Libya imekuwa ikijitetea mbele ya baraza la haki za binadamu dhidi ya madai ya utekelezaji wa uhalifu wa kivita. Libya ambayo ilisitishwa uanachama kwenye baraza hilo mapema mwaka huu ,imepewa fursa ya kuzikilizwa kufuatia kuchapishwa kwa ripoti ya tume ya kimataifa ya uchunguzi ambao ulihitimisha kwamba uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita umetekelezwa na vikosi vya serikali Libya.Ripoti inasema vikosi vya serikali viliwalenga kwa makusudi raia na kujihusisha na mauaji, kuwafunga, kuwatesa, kuwatowesha kwa nguvu na ubakaji.

Mkuu wa ujumbe wa serikali ya Libya Mustafa Shaaban amesema serikali yake imekuwa ikikabiliwa na wanamgambo na badala ya kuwashutumu wao washutumu makundi ya upinzani na vikosi vya kimataifa vinavyotekeleza azimio la Umoja wa Mataifa kwa ukiukaji wa haki za binadamu. Sherif Bassiouni aliongoza tume ya kimataifa ya uchunguzi.

(SAUTI YA SHERIF BASSIOUNI)