Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari vinaendelea Darfur:Ocampo

Uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari vinaendelea Darfur:Ocampo

 

Uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari vinaendelea kwenye jimbo la Darfur Sudan amesema mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC bwana Luis Moreno Ocampo.

Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Darfur Ocampo amesema mashambulizi dhidi ya makundi ya kabila la Fur, Massalit na Zaghawa ambayo yalianza mwaka 2003 bado yanaendele.

Bwana Ocampo amelikumbusha baraza kwamba Rais wa Sudan Omar Al Bashir anatafutwa na mahakama ya ICC kwa makosa ya uhalifu unaohusiana na mauaji ya watu wa makundi hayo.

(SAUTI YA MORENO OCAMPO)

Uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari vinaendelea Darfur. Mashambulizi ya anga dhidi ya raia na mauaji ya moja kwa moja ya watu wa makabila haya yanaendelea.

Watu wengi wa makabila ya Fur, Zaghawa na Massalit sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi. Mamilioni ya watu hawa waliotawanywa pia wanakabiliwa hii leo na ubakaji, ugaidi, hali ya maisha iliyo na lengo la kusambaratisha jamii zao na mauaji ya kimbari.