UM waitaka China kuheshimu haki za binadamu
Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa lenye shabaya ya kutekelezwa kwa maazimio kadhaa limeitolea mwito China kubainisha mahala inapowashikilia watu kadhaa ikiwemo wafuas wa mrengo wa Tibet walilokamatwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana.
Mapema mwezi April mwaka huu, serikali ya China iliwakamata watu zaidi ya 300 wa mafungamano ya Ngaba Kirti na ya kupelekwa katika sehemu isiyojulikana hadi sasa. Tukio hilo linadaiwa kuendeshw ana vikosi vya polisi vikishirikiana na Kikosi cha usalama wa taifa na Jeshi la Ukombozi wa China.
Ikielezea tukio hilo, Umoja wa Mataifa umeitaka mamlaka China kutoa taari za
kweli juu ya tukio hilo na kueleza bayana mahala inapowashikilia watu hao.
Wataalamu hao wameionya China kuwa inawajibika kuheshimu na sheria za kimataifa
juu ya haki za binadamu.