Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha siku ya bahari duniani kwa vizazi vijavyo

UM waadhimisha siku ya bahari duniani kwa vizazi vijavyo

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki moon ametoa wito kwa serikali na watu kuhakikisha kuwa bahari zilizo ulimwenguni zimelindwa akisema kuwa zinakabiliwa na hatari kubwa. Akiongea wakati wa maaadhimisho ya siku ya bahari duniani ambayo inaadhimishwa hii leo kote duniani Ban amezungumzia kile alichokitaja kama matatizo yanayokumba bahari yakiwemo uvuvi kupita kiasi , athari za mabadiliko ya hali ya hewa , hali ya wafanyikazi wa habarini na uhamiaji kupitia baharini. Ban amesema kuwa shughuli na sera zinazohusiana na bahari zinahitaji kuzingatia masuala matatu yakiwemo mazingira , masuala ya kijamii na kiuchumi ambapo alishauri kila serikali kuchukua jukumu kulinda mazingira ya bahari.