Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwimbaji Moore ateuliwa balozi mwema katika kuwakumbuka waathiriwa wa biashara ya utumwa

Mwimbaji Moore ateuliwa balozi mwema katika kuwakumbuka waathiriwa wa biashara ya utumwa

Mwimbaji na pia mcheza filamu Melba Moore ameteuliwa kuwa balozi mwema katika kuweka kumbukumbu ya kuwakumbuka waathiriwa wa biashara ya utumwa ya Transatlantic. Kumbukumbu itaweka kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kama ishara ya miaka 400 ya biashara ya utumwa kwa waafrika waliopelekwa kwenye nchi za Caribbean na Marekani.

“Nimefurahishwa kwa kuteuliwa balozi mwema wa kumbukumbu kwenye Umoja wa Mataiafa kwa heshima kwa waathiriwa wa biashara ya utumwa. Kwa kuwa nitawawakilisha na kuongea kwa niaba ya watu wengi kutoka kila upande hasa kwenye biashara , watu mashuhuri na vyombo vya habari ili niweze pia niweze kuinua sauti yangu kwa kuimba kwa sasa na baadaye”.

Melba Moore ataungana katika jitihada zake na wanachama wa kikundi cha muziki aina ya Reggae cha Morgan Heritage aliye pia abalozi mwema kwenye kumbukumbu hiyo.