Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa Ukingo wa Gaza unazidi kuzorota-Ripoti

Uchumi wa Ukingo wa Gaza unazidi kuzorota-Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika wakimbizi wa Palestina imeonyesha kukwama kwa hali ya utengamao wa ustawi na kuanguka kwa hali ya uchumi wa ukingo wa Gaza.

Ripoti hiyo imesema kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kiliongezeka zaidi katika muhula wa pili wa mwaka 2010 na kusababisha pia uwezo wa watu kumudu maisha yao kwenye soko kunguka zaidi.

Viashirio ndani ya utafiti huo vinaonyesha kuwa kumekuwa na hali ngumu zaidi hasa katika maeneo yanayokaliwa na wakimbizi tofauti na maeneo yasiyo na wakimbizi.

Ripoti hiyo imekosoa taarifa za vyombo vya habari vilivyosema kwamba hali ya uchimi katika eneo la ukingo wa Gaza imeimarika kwa kiwango cha kuridhisha.