Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Panama yawa ya kwanza kuridhia mkataba kimataifa

Panama yawa ya kwanza kuridhia mkataba kimataifa

Panama imekuwa nchi ya kwanza duniani kuridhia mkataba wa kimataifa unaoondosha dhana ya taifa na hivyo kukaribisha hatua itayowasaidia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na tatizo la kukosa taifa.

Mkataba huo nambari 1954 unatoa maelekezo yanayotaka kila nchi kuwa na utashi wa kiutendaji kwa watu ambao wamekosa makwao. Eneo kubwa linalozingatiwa na mkataba huo ambao umegawika kwenye vipengele 66,ni kuziomba nchi kutowabagua watu hao kwenye utoaji wa huduma za matibabu na masuala ya kisheria.

Tayari shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepongeza hatua hiyo iliyofikiwa na Panama ikisema kuwa kwani inafungua milango kwa mamia ya watu ambao hawana makwao.

Aidha UNHCR imesema inaamini mataifa mengine yatafuata mkondo huo uliochukuliwa na Panama.