Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gharama za matibabu katika nchi zinazoendelea ni changamoto:UM

Gharama za matibabu katika nchi zinazoendelea ni changamoto:UM

Gharama ya matibabu hasa katika mataifa yanayostawi imetajwa kama changamoto kubwa katika vita dhidi ya magonjwa.

Kukabiliana na magongwa ni miongoni mwa malengo ya maendeleo ya milenia yaliyoainishwa na Umoja wa Mataifa baada ya wakuu wa nchi kuyapitisha mwaka 200, lakini imebainika kuwa watu wanaoishi katika umaskini wanaendelea kulemewa na mzigo wa kugharamia matibabu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa bima ya matibabu  ni muhimu lakini sio mataifa yoye yanayomudu kuhakikisha hilo kwa watu wake.

Kwenye mkutano wa kimataifa wa afya mjini Mombasa Kenya bima ya afya kwa mataifa mbali duniani imejadiliwa kwa mapana na wajumbe na wataalamu wa afya kutoka nchi 15 wanaohudhuria kongamano hilo  .

Mwanahabari Josephat Kioko amezungumza na Daktari wa miaka mingi nchini Kenya Professor Richard Otieno Muga, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa bodi ya Bima ya matibabu -N.H.I.F katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

(MAHOJIANO NA DR MUGA)