Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM ataka raia nchini Iraq kupewa usalama zaidi

Afisa wa UM ataka raia nchini Iraq kupewa usalama zaidi

Naibu katibu mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Ivan Šimonović ameishauri serikali ya Iraq kujitahidi zaidi katika kuwalinda raia wake .

Akiongea baada ya kukamilisha ziara yake ya siku kumi nchini Iraq Šimonović amesema kuwa ni muhimu iwapo serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa raia wamelindwa na pia kuhakikisha kuwa yeyote ambaye atahusika kwenye vitendo vya ghasia amechukuluwa hatua za kisheria.

Afisa huyo amelaani visa vya kutoweka kwa watu , kufungwa na kuteswa visa ambavyo vimeripotiwa kote nchini Iraq. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)