Watu zaidi waendelea kuuawa kwenye ghasia nchini Yemen:WHO

7 Juni 2011

Inakadiriwa kuwa watu 29 waliuawa nchini Yemen kufuatia mapigano makali wiki iliyopita huku ile ya waliokufa tangu kuanza kwa mzozo nchini humo ikikadiriwa kuwa watu 262 na wengine 3,287 wakijeruhiwa.

Shirika la afya duniani WHO limetuma tani 20 za madawa kwenye mji mkuu Sanaa kutoka ghala lake mjini Dubai. WHO inasema kuwa imeweka wafanyikazi nchini Yemen na kuongeza kuwa kutokana na ghasia zinazoendelea watu zaidi wanahitaji matibabu na misaada ya kibinadamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter