Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito wa kutaka kukamatwa kwa Goran Hadzic watolewa

Wito wa kutaka kukamatwa kwa Goran Hadzic watolewa

Mwendesha mashtaka kwenye mahakama ya uhalifu ya iliyokuwa Yugoslavia anasema kuwa Goran Hadzic ambaye ni raia wa Serbia anayedaiwa kuhusika kwenye uhalifu wa kivita uliotokea nchini Croatia mapema miaka ya tisini anastahili kukamatwa bila kukawia.

Hadzic mwenye umri wa miaka 50 anashutumiwa kwa kuhusika katika mauaji ya raia wa Croatia, kurejeshwa makwao kwa karibu watu 28,000 wasiokuwa wacroatia kutoka Croatia wakati wa vita nchini humo kati ya mwaka 1991 na 1995.

Mwendesha mashtaka huyo pia anaishauri serikali ya Serbia kujitolea na kuchunguza mtandao uliomuunga mkono Ratko Mladic mshukuwa mwingine wa uhalifu wa kivita aliyekamatwa mwezi Mei mwaka huu.