Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha hatua zilizopigwa kwenye makubaliano ya amani Darfur

Ban akaribisha hatua zilizopigwa kwenye makubaliano ya amani Darfur

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amekaribisha hatua zilizopigwa wakati wa mazunguzmo ya kutafuta amani kwa mzozo wa miaka minane kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan na kutoa wito kwa pande husika kuchukua hatua zifaazo ili kupatikane amani ya kudumu.

Kwenye mkutano wa washikadau kwenye jimbo la Darfur ulioandaliwa mjini Doha nchini Qatar wajumbe waliunga mkono kutiwa sahihi kwa makubaliano ambayo yatasitisha mapigano na kuleta amani. Wajumbe hao walisema kuwa hatua zimepigwa kwenye masuala kadha yakiwemo ya ugavi wa mamlaka, usimamizi , haki za binadamu , fidia na kurejea makwao kwa wakimbizi wa ndani na pia wakimbizi wa kawaida.