Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yatoa tuzo kwa washindi wa ubunifu kwenye utalii

UM yatoa tuzo kwa washindi wa ubunifu kwenye utalii

Mpango ulioendeshwa huko Slovenia wa ujenzi wa hoteli zinazotoa fursa kwa watu wenye ulemavu kupita kwa urahisi ndani ya majengo yake, pamoja na hatua iliyochukuliwa huko Australia ambayo inaruhusu watu kujitolea ili kulinda uharibifu wa kibilojia, ni baadhi ya maeneo ambayo yametwaa tuzo ya Umoja wa Mataifa inayohimiza ubunifu unaokuza utalii.

Tuzo hiyo ya mwaka huu 2011 imetolewa kwenye hafla maalumu iliyofanyika nchini Ureno na kuhudhuriwa na washiriki mbalimbali ikiwemo taasisi za kiserikali pamoja na binafsi.

Tuzo hiyo imeratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii UNWTO.  Mashirika kadhaa ya kiraa yamejitwalia tuzo inayozingatia uhifadhi za mazingira wakati shirika la Slovenia likiondoka na tuzo juu ya afya.