Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amesema itakuwa ni heshima kubwa kupata fursa ya kuongoza UM kwa awamu ya pili

Ban amesema itakuwa ni heshima kubwa kupata fursa ya kuongoza UM kwa awamu ya pili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo asubuhi ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba ana nia ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa muhula mwingine.

Ban amesema amepeleka barua kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na kwenye baraza za usalama akiomba kufikiriwa kwa muhula wa pili na amesema imekuwa heshima kubwa kwake kuongoza Umoja huu na akipewa fursa atakuwa tayari kuongoza tena.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban pia amegusia jinsi walivyojitahidi kuwasaidia wasiojiweza katika kipindi hiki cha mdororo wa uchumi, na kutoa kauli kuhusu machafuko katika ulimwengu wa Kiarabu na Afrika Kaskazini ambako wamewataka viongizi kuheshimu matakwa ya walio wengi, pia amesema juhudi zaidi zinatakiwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015.

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa anateuliwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa mapendekezo ya baraza la usalama, hivyo uchaguzi wa Katibu mkuu unaweza kupigiwa kurura ta turufu na mjumbe wowote wa kudumu wa baraza la usalama. Ban ambaye ni Katibu mkuu wa nane wa Umoja wa Matifa aliingia madarakani Januari mosi 2007 na hadi sasa hakuna aliyejitokeza kuchuana naye katika awamu hii ya pili ya uongozi.