Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR ametaka kuwepo nyezo kushughulikia wanaotawanyishwa na mabadiliko ya hali ya hewa

Mkuu wa UNHCR ametaka kuwepo nyezo kushughulikia wanaotawanyishwa na mabadiliko ya hali ya hewa

Dunia inahitaji haraka njia mpya ya kukabikliana na majanga ya asili na wakimbizi amesema kamishina mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR, Antonio Guterres.

Bwana Guterres ameyasema hayo leo miji Oslo na kuzitaka nchi kuchukua hatua mpya za kushughulikia wakimbizi wa ndani na nje wanaolazimika kuwa katika hali hiyo kutokana na hali ya hewa.

Katika mkutano huo wa Nansen unaojadili mabadiliko ya hali ya hewa na wakimbizi katika karne ya 21, umelielezea suala hilo kama ni chsngamoto kubwa na hakuna suluhisho lingine isipokuwa ari ya kisiasa ya kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa amesema Gutteres. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)