UNMIS imezitaka pande husika kusitisha mvutano Abyei na jimbo la kusini la Kordofan

6 Juni 2011

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMIS unahofia hali ya mvutano inayoendelea kwenye jimbo la Abyei na Kordofan na umezitaka pande zote kuzuia kuendelea kwa machafuko zaidi ambayo yatasababisha maisha zaidi ya raia kupotea.

Katika eneo la Abyei uporaji unaendelea licha ya jeshi la Sudan SAF kutoa hakikisho la kusitisha vitendo hivyo. UNMIS imelitaka pia jeshi la Sudan kuwaachilia raia wote ambao bado wanashikiliwa na kutoa fursa ya wafanyakazi wa misaada kwenye maeneo yote ya Abyei kuhakikisha kama kuna raia wanaohitaji msaada ili wasaidiwe na kupewa ulinzi.

UNMIS imesema kitendo cha jeshi la SAF kuvurumisha makombora kutoka kwenye kituo cha Umoja wa mataifa lazima kikome kwani ni tishio kubwa kwa uwepo wa Umoja wa mataifa, doroa na helikopta zinazopaa na kutua Abyei na pia ni hatari kwa mamia ya raia ambao wako tayari kurejea makwao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter