Unicef imesisitiza haja ya kumchanja kila mtoto

6 Juni 2011

Wakati viongozi wa dunia wakijiandaa kukutana London kwa muungano wa GAVI kwenye mkutano wiki ijayo , shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limewatolea wito wahisani kufadhili juhudi za kimataifa za chanjo ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watoto ilifikapo 2015.

UNICEF imesisitiza kwamba matumizi bora ya msaada wa fedha za chanjo ni kutekeleza mipango ambayo inatoa kipaumbele kwa watoto ambao ni vigumu kuwafikia na ambao kwa sasa wanakosa chanjo tano ambazo ni muhimu. Hivi sasa mtoto mmoja kati ya watano hajachanjwa amesema mkurugenzi mkuu wa UNICEF Antony Lake. Jason Nyakunsi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud