Usalama wa nyuklia ni muhimu katika maisha na maendeleo:IAEA

6 Juni 2011

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukiya Amano amesema usalama wa nyukilia ni muhimu sana kwa maisha ,afya na maendeo ya binadamu huku wakitumia sayansi ya nyuklia hitio kwa maendeleo.

Amesema katika upande wa afya vita dhidi ya saratani katika nchi zinazoendelea vinaendelea kupewa uzito wa juu, wakati katika upande wa chakula la afya shirika la IAEA zinazisaidia nchi kadhaa katika mikakati ya kitaifa ikiwemo Senegal. Amano aliyekuwa akitoa taarifa kwenye bodi ya magavana mjini Vienna Austria kwenye makao makuu ya IAEA amezikumbusha nchi wanachama jinsi ilivyo muhimu kuchangia kikamilifu na kwa wakati kwenye mfuko wa ushirikiano wa kiufundi. Amesema kwa mwaka 2010 miradi ya matumizi ya amani ya nyuklia ilikuwa chanzo cha ufadhili wa miaradi.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)

Katika taarifa yake pia amegusia matokeo ya timu iliyokwenda kwenye mtambo wa Fukushima Daiichi Japani, nyuklia ya Iran, jamhuri ya Korea DPRK, na Syria.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter