Ban ahofia hali inayoghubika eneo linalokataliwa la Syria milima ya Golan

6 Juni 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye amekuwa akifuatilia hali ya eneo la Syria linalokaliwa na milila ya Golan amesema anatiwa hofu na matukio yanayoendelea ikiwa ni pamoja na taarifa za watu kutaka kuvuka uzio wa Israel na idadi iliyojulikana ya raia waliouawa kwa risasi.

Vikosi vya Umoja wa mataifa katika eneo hilo UNDOF inatafuta kuthibitisha taarifa hizo na kujaribu kurejesha utulivu katika eneo hilo. Ban amesema anasikitishwa na vifo vya watu na ametuma salamu za rambirambi kwa familia na waliojeruhiwa na kupoteza maisha.

Amelaani matumizi ya ghasia na vitendo vyovyote vya kuchochea machafuko na kusema matukio yanayoendelea sasa na yaliyotokea May 15 yanaweka mkataba wa amani njia panda tena. Ban amezitaka pande zote kujizuia na kuheshimu sheria za haki za binadamu za kimataifa za kuhakikisha raia wanalindwa.Pia ameikumkbusha serikali ya Syria wajibu wake wa kuwalinda wafanyakazi wa UNDOF na ofisi zao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud