Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawaokoa wahamiaji waliokwama kwenye jangwa la Chad

IOM yawaokoa wahamiaji waliokwama kwenye jangwa la Chad

Kundi kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji IOM lililoondoka mjini Faya baada ya ripoti kuwa kulikuwa na wahamiaji zaidi ya 60 wakiwemo wanawake na watoto wanaoikimbia Libya walikuwa wamekwama kwenye eneo la Zourake baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupatwa na matatizo ya kimitambo limefanikiwa kurejea Faya pamoja na wahamiaji hao.

Kulingana na Craig Murphy afisa wa duduma katika shirika la IOM ni kuwa wanawake 21 na watoto walisafirishwa na lori lilokuwa likipita huku wengine 46 wakisafiri umbali wa kilomita 295 wakitumia lori la IOM. Mmoja wa wale aliyekuwa amekwama kwenye eneo la Zouraké kwa muda wa siku sita bila maji alisema kuwa alikuwa mfanyikazi kwenye kampuni moja ya mafuta kwenye mji mdogo ulio karibu na mji wa Benghazi nchini Libya na wakati akiondoka hakuwa amelipwa mshara wake wa miezi sita.