Mladic afikishwa mahakami kujibu mashataka ya uhalifu wa kivita

3 Juni 2011

Kesi inayomkabili mshukiwa wa uhalifu wa kivita Ratko Mladic iling’oa nanga hii leo mjini Hague ambapo alisomewa mashataka yanayomkabili mashataka ambayo aliyakanusha. Mladic anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita alioutekeleza pamoja na vikosi vyake kwenye ghasia zilizoikumba Bosnia na Herzegovina toka mwaka 1992 hadi 1995.

Mladic alikuwa afisa wa ngazi ya juu jeshini nchini Boasnia wakati wa vita nchini Bosnia na Herzegovina. Frederick Swinnen ni mshauri wa mwendesha mashtaka kwenye mahakama hiyo.

(SAUTI YA FREDERICK SWINNEN)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter