UM wataka Australia kuwalinda watoto wanaotafuta hifadhi

3 Juni 2011

Mipango ya Australia ya kukabilina na wahamiaji haramu kwa kuwarejesha wahamiaji walio na umri mdogo wasioandamana na wakubwa wao kwenye kituo wanakozuiliwa nchini Malaysia imeshutumiwa vikali na Umoja wa Mataifa.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na lile la kuwahudumia watoto la UNICEF yanasema kuwa hayakufahamishwa kuhusu mipango hiyo mapema. Sasa mashirika hayo yanataka kujua ni hatua zipi zimechukuliwa na serikali za Australia na Malaysia kuwalinda watoto kwenye vituo hivyo. Adrian Edwards ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud