Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa uchumi unaojali mazingira UM umezindua juhudi kuwapa umeme nchi masikini

Kwa uchumi unaojali mazingira UM umezindua juhudi kuwapa umeme nchi masikini

Baadhi ya makampuni makubwa yanayoongoza kwa nishati ya umeme duniani yanashirikiana na Umoja wa Mataifa kutafuta njia za kuwapa nishati ya umeme watu bilioni 2.5 duniani ambao hawana nishati hiyo.

Wakurugenzi kutoka kundi la makampuni manane liitwalo e8 limewsili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York hii leo wakiwa kwenye magari 13 yanayotumia umeme ili kuonyesha jinsi gani umeme ulivyo na matumizi mbalimbali.

Pia wakurugenzi hao wametaka kuweka msisitizo wa umuhimu wa makampuni ya umma kushirikiana na kufanya kazi pamoja na mashirika ya umma. Mike Morris ni mwenyekiti wa shirika la umeme la Marekani na ni miongoni mwa wakuu hao waliwasili Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA MIKE MORRIS)

“Suala zima la ushirikiano baina ya mashirika binafsi na ya umma ni japo ambalo e8 na Umoja wa mataifa wanalitilia maanani, mnaposhirikiana katika Miradi ili kuwapa umee duniani watu ambao hawakuwa nao hapo awali mnaleta mabadiliko makubwa katika maisha yao na fursa za maendeleo.”