Watu waliosafirishwa kinyume na sheria wasichukuliwe kama wahamiaji wasiofuata sheria: UM

2 Juni 2011

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na usafirishaji haramu wa binadamu Joy Ngozi Ezeilo amesema kuwa watu wanaosafirishwa kiharamu wanastahili kuhudumiwa kama watu ambao haki zao zimekiukwa na wala sio vyombo vya uchunguzi vua uvunjaji wa sheria.

Akiongea alipowasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Ezeilo amesema kuwa watu waliosafirishwa kiharamu mara nyingi huwa wanachukuliwa kama wahamiaji wasiofuata sheria ambapo wanakamatwa na kurudishwa makwao bila ya kupatiwa fursa ya kuomba usaidizi.

Wengi wanaosafirishwa kiharamu mara nyingi hawalipwi fidia kwa kuwa hawana njia ya kupata habari wala usaidizi wa kisheria na mahitaji mengine ya kuwasaidia kulipwa fidia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter