Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano utakaoandaliwa mjini Mogadishu ni fursa ya mwisho kwa nchi hiyo: Mahiga

Mkutano utakaoandaliwa mjini Mogadishu ni fursa ya mwisho kwa nchi hiyo: Mahiga

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga amesema kuwa mkutano unaotarajiwa kuandaliwa mjini Mogadishu mwezi Juni utakuwa fursa ya mwisho kwa wasomali kuafikia makubaliano ili nchi hiyo iweze kusonga mbele kisiasa.

Akiongea na vyombo vya habari Mahiga amesema kuwa suala la Somalia litakabidhiwa Umoja wa Mataifa iwapo viongozi nchini humo watashindwa kuafikia makubaliano kwenye mkutano huo.

Mahiga pia amesema kuwa eneo lililojitenga la Somaliland halitahudhuria mkutano huo kwa kuwa eneo hilo lilikuwa limekubaliana kushirikiana tu na sehemu zingine za Somalia katika masuala kama uharamia na usalama.