Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu la UM lajadili uchumi unaojali mazingira

Baraza kuu la UM lajadili uchumi unaojali mazingira

Baraza la kuu la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili uchumi unaojali mazingira katika maandalizi ya mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu utakaofanyika mwaka ujao.

Akizungumza kwenye mjadala huo naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro Amesema mkutano ujao wa Rio+20 una malengo makuu matatu ambayo ni kuimarisha ari ya kisiasa katika kuleta maendeleo endelevu, kutathimini hatua zilizopigwa na mapungufu yaliyopo na kushughulikia changamoto mpya na zinazoendelea kujitokeza.

Mkutano huo pia una mada mbili ambazo ni uchumi unaojali mazingira kwa ajili ya maendeleo na kutokomeza umasikini na pili ni mfumo maalumu kwa maendeleo endelevu. Ameongeza ingawa kuna mafanikio kiasi katika kupunguza umasikini hasa Asia kwa kuboresha elimu, afya na usawa wa kijinsia, kupunguz ukataji miti na kuanzishwa mkataba wa Nagoya kuhusu bayo-anuai bado kuna mapungufu.

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)

Amesema kila nchi inapaswa kutanabahi ni jinsi gani uchumi unaojali mazingira utafanya kazi kwa watu wake.